WAKATI wanamuziki Bongo wakiendelea kuiga wanamuziki kutoka
nje na kusahau kabisa muziki wao wa asili, wasanii wa Nigeria wamekuwa
mfano wa kuigwa kwa kuimba nyimbo zenye vionjo vya ngoma zao za asili
huku mwanamuziki Chinedu Okoli ‘Mr Flavour’ akiongoza kwenye listi hiyo.
Mwimbaji huyu mwenye ‘body’ la kutosha,anatajwa kupenda kufanya
muziki wa asili ya makabila mbalimbali ya Nigeria kupitia baadhi ya
nyimbo zake kama vile Nwa Baby, Adamma, Ololufe, Uyi, Ada Ada na
nyingine nyingi.
Flavour anajulikana sana Bongo kupitia wimbo wake wa Ashawo ambao
ulimpa umaarufu mkubwa kabla ya Wimbo wa Nana alioshirikishwa na Msanii
Diamond Platnumz huku staili yake ya kucheza kifua wazi kwa kukata mauno
ikimtofautisha na wasanii wengi wa levo yake.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment