Dk. Fadhili Emily.
KASI ya Rais Dk. John Pombe Magufuli inatikisa kila kona. Baada ya
mtabibu Dk. Juma Mwaka ‘JJ Mwaka’ kuibukiwa hospitalini kwake na Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hamis
Kigwangalla wiki iliyopita na kuagizwa uchunguzi wa uhalali wa huduma
zake, hali imekuwa tete kwa mtatibu mwingine, Dk. Fadhili Emily
anayemiki kliniki ijulikanayo kama The Fadhaget Sanitarium iliyopo
Afrikana Mbezi Beach jijini Dar.
Chanzo makini kimeweka wazi kuwa Dk. Fadhili amepata taarifa kuwa tumbuatumbua ya Magufuli itamfikia, kwani tayari TRA wameshamweka kwenye ‘tageti’ zao na muda wowote watamkagua ili kujiridhisha kama mali alizonazo anamiliki kihalali na kama analipa kodi stahiki.
“Dokta ameshapewa hizo taarifa. Lazima atakuwa tumbo joto, maana si
unajua kila mtu anatilia shaka ule utajiri wake, haufanani hata kidogo
na umri wake.
“Daah! Jamaa ni noma. Ana nyumba za ghorofa zaidi ya tatu Mbezi Beach halafu zote za gharama. Ana magari ya kutembelea matatu yote ya gharama; Toyota MRS, Toyota Land Cruiser V8 na Toyota Celca.
“Katika hiyo mijengo mitatu, moja anaishi yeye, lingine amepanga
kuweka TV yake maana anataka kufungua kituo cha runinga na nyingine
wanakaa wafanyakazi wake na tena ana vitu vingi tu ambavyo anavifanya
siri,” kilisema chanzo hicho.
Jitihada za kumpata Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata ziligonga
mwamba lakini hata hivyo alipatikana mmoja wa maofisa wa mamlaka hiyo
ambaye aliomba jina lake lisichorwe gazetini, kwa kuwa si msemaji ambapo
alisema wao kama mamlaka, wamedhamiria kukusanya kodi kadiri
iwezekanavyo hivyo kama Dk. Fadhili naye amekwepa, watamfikia.
“Tumedhamiria kwa dhati kwenda na kasi ya Dk. John Pombe Magufuli
rais wetu. Hakuna atakayekwepa kodi halafu tusimfikie. Niwasihi wote
ambao wamekuwa wakikwepa kodi, walipe mapema kabla hatujawafikia,”
alisema afisa huyo.
Gazeti hili lilimtafuta Dk. Fadhili kwa njia ya simu, alipopatikana na kusomewa madai hayo ya utajiri wake kutiliwa shaka, alisema hata yeye amesikia kuwa TRA pamoja na mamlaka nyingine zinamchunguza ili ikibainika amefanya ubabaishaji sehemu wamtumbue.
“Ninazo hizo taarifa lakini labda tu nikwambie, mimi sina kitu hata
kimoja cha magumashi. Nimeanza kutoa huduma ya kitabibu kwa miaka mingi
iliyopita kuliko hata hao madokta maarufu mnaowasikia wakijitangaza.
“Mimi simkimbii mtu katika hospitali kama wao. Nipo muda wote,
nikitoka labda liwe ni suala la kazi maana nina matawi mengi mikoani
huwa naenda pia kutoa huduma,” alisema Dk. Fadhili.
0 comments:
Post a Comment