IKIWA zimepita siku chache baada ya
rappa machachari kutoka Marekani Meek Mill amvalishe pete ya dhahabu
mpenzi wake Nick Minaj kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa hivi
karibuni wapendanao hao wameibua ‘headline’ kwenye Mtandao wa Kijamii
wa Twitter baada ya Nick kuwauliza maswali mashabiki wake juu ya mahali
pa kufanyia harusi hiyo akilenga ufukweni au kanisani.
Baada ya Nick, 33, kupost maswali hayo
ndani ya muda mchache zaidi ya mashabiki wake 20,000 walitoa maoni yao
huku kati yao 11, 600 walipendekeza ndoa ya wawili hao kufanyikia beach.
Hata hivyo Nick alionekana kuchukua
maoni ya mashabiki wake baada ya kuwajibu kuwa atayafanyia kazi kwa
‘kudiscuss’ na Meek jambo linaloonyesha kuwa ndoa ya waoendanao hao
inanukia.
RT for beach wedding. Fave for church wedding.
— NICKI MINAJ (@NICKIMINAJ) December 27, 2015

0 comments:
Post a Comment