KAMA UNA MPENZI NA ANAYAFANYA HAYA BASI ANDIKA UMEUMIA!

Kujua kama fulani ana wengine au la,ni kuangalia namna ambavyo anakuwa wazi kwako.Ni uwazi wa namna gani ninaouzungumzia? Ni hasa katika suala zima la mawasiliano.Ukiwa na mtu halafu simu yake inakuwa shida kuishika,au ukiishika anauliza ya nini? Hesabu umeumia.

Yeyote ambaye ana masharti katika simu yake ya mkononi,jua kwa asilimia kubwa si mwaminifu.Unaweza kumdanganya mwenzi wako kwa namna unavyojua,lakini huu ni ukweli kwamba ukiona mtu hana imani na simu yake huyo kwa asilimia kubwa si mwaminifu.

Hakuna kazi ambayo unaweza kufanya ikiwa ni ya siri sana kiasi kwamba hata mkeo au mumeo asijue.Hata kama ni Usalama wa Taifa,kabla ya kuoa ipo fomu anbayo mwanamke anapaswa kuijaza na anapaswa kufahamu mumewe au mkewe ni mtu mwenye kufanya kazi gani.

Najua iko kazi moja ambayo ndiyo pekee wakati mwingine inakuwa hurusiwi kabisa kuoa,lakini kwa mtu yeyote ambaye yuko kwenye ndoa na anasema ana mambo ya siri hawezi kumweleza mkewe au mumewe,kwa asilimia kubwa ni kudanganyana.

Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa wanaume au wanawake wanatoka nje si kwa sababu hawazipendi ndoa zao au kwamba wako tayari kwa talaka.Bali wengine wanatoka nje kwa sababu tu ya kero ndani ya nyumba kwahiyo wanakwenda nje wakiamini watapata amani,au wengine ni kwa sababu ya umaskini,wanakwenda huko wakiamini watapata hiki na kile ambacho wanakikosa ndani.
Hivyo inashauriwa kuwa ni muhimu kwa wapenzi kuangalia namna ya kuimarisha uhusiano baina yao.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment