Nimekuwa mmoja wa wajumbe wa kamati ya ushindi kwenye kampeni ktk jimbo flani ambalo lipo ndanindani sana, baada ya kukaa kwa kwa zaidi ya mwezi nikiwa nje ya mji juzi wife kaja kunitembelea akiwa kaongozana na mke wa mgombea maana familia zetu marafiki, tena ujio wao ni wa kushtukiza bila taarifa (cku umepandishwa daraja wanasema alini surprise)
Mwanzo tulipoonana alikuwa ni mtu mwenye bashasha tena aliyejawa muwashawasha, nikajua hapa leo kazi ni moja kuviringishana mwanzo mwisho usiku baada ya msosi yeye akatangulia kulala sisi tukabaki na vikao vyetu vya mikakati, saa 6 hivi naingia chumbani namkuta kakaa kitandani amefura kwa hasira hadi nikapata hofu (hapo nikaona lile tumaini la kuviringishana linayeyuka taratibu)
Tangu siku hiyo hadi alipondoka cku mbili baadae tulikuwa tunalala na nguo tu, hakuna maelewano jamani hebu nipeni vi mbinu viwili vi3 vya kumlainisha huyu mtu ikiwemo uongo wa level za juu maana naona anaelekea kufika kiwango cha mwisho cha uvumilivu wake, nitamkosa hivi hivi hii ni serious jamani.

0 comments:
Post a Comment