Mrembo Amtibu AUNTY Kitambi!

aunt
Imelda Mtema
MREMBO aliyejulikana kwa jina la Fatina Deus, ‘Fettylicious’ amesema  amempa bure tiba ya kitambi staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel ili kumuondolea kero aliyokuwa akiipata. 

Akipiga stori na gazeti hili, Fettylicious alisema miongoni mwa watu waliokuwa wakisumbuka na tatizo la kuwa na kitambi  ni Aunt lakini kwa kuwa yeye lengo lake ni kuwasaidia mastaa wengi, amempa Aunt bure dawa hiyo ili wengine wamtafute. 
“Nimempa dawa ya asili kabisa ya kuondoa tumbo ambalo ni kero kwa warembo wengi, Aunt atapona na ninawashauri na mastaa wengine wanione ili waondokane na aibu ya kuwa na matumbo utadhani wajawazito,” alisema Fettylicious.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment