Lagos, Nigeria
STAA wa Pop nchini Nigeria anayetamba na Wimbo wa Dodo, Davido, ameweka wazi msimamo wake wa kutotaka kuigiza filamu tena. Hivi karibuni staa huyo aliweka historia mpya ya kufanya vizuri kwenye moja ya filamu za Nigeria Nollywood aliyoigiza yenye jina la John Zerebe ikiandaliwa na binamu yake, Ikey Ojeogwu,
Davido amesema kuwa, John Zerebe itakuwa ndiyo filamu yake ya kwanza na ya mwisho kwake kuigiza. Ameongeza kuwa hana mpango wa kuigiza tena kama baadhi ya watu wanavyomuomba, maana malengo yake si kuwa muigizaji.
“Hicho ni kitu ambacho sitofanya, sidhani kama nitacheza filamu tena tofauti na hii ya John Zerebe Part 2”, alisema Davido.
0 comments:
Post a Comment