Selfie ya Miss Universe Israel na Miss Lebanon yazua mgogoro mkubwa wa kisiasa katika nchi zao!

Kuanzia kushoto ni Miss Israel, Doron Matalon, Miss Japan, Miss Slovenia na Miss Lebanon, Saly Griege 
Kwanini selfie ya wasichana warembo inaweza kugeuka kuwa issue ya kimataifa? Labda pale tu Israel na Lebanon zinapohusika. 

Timbwili hilo lilianza wiki iliyopita baada ya mwakilishi wa Miss Universe Israel, Doron Matalon kupost picha kwenye Instagram akiwa na warembo wengine watatu akiwemo Miss Lebanon, Saly Griege na wengine wa Japan na Slovenia.  

Picha hiyo ikaleta shida kubwa nchini Lebanon yenye sheria inayowakataza wananchi wake kujumuika na Waisrael.
Mwaka 1993, serikali ya Lebanon ilimuondoa mwakilishi wake kwenye shindano la Miss Universe, Ghada al-Turk baada ya shirika la Agence France Press kusambaza picha inayomuonesha akifurahi pamoja na mshiriki wa Israel.
Kwa upande wake, Griege alidai kuwa hakutarajia kama mwakilishi huyo wa Israel angetokea kwenye picha hiyo. “I was very cautious to avoid being in any photo or communication with Miss Israel (that tried several times to have a photo with me) … I was having a photo with Miss Japan, Miss Slovenia and myself; suddenly Miss Israel jumped in, took a selfie, and put it on her social media,” alijitetea mrembo huyo. 

Matalon naye alijibu kwenye ukurasa wake wa Facebook akidai kuwa majibu ya Griege hayajamshangaza ila yamempa huzuni.
“Too bad you cannot put the hostility out of the game, only for three weeks of an experience of a lifetime that we can meet girls from around the world and also from the neighbouring [sic] country,” aliandika.
feature2
Gazeti la New York Post limedai kuwa serikali ya Lebanon inafanya uchunguzi kuhusu picha hiyo. Shindano la Miss Universe litafanyika jijini Miami, Florida nchini Marekani, Jumapili ijayo.
  HII NDIO ZAWADI YA RAY C KWA RAIS JAKAYA KIKWETE!
===>>SOMA ZAIDI HAPA!
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA
KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO
TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment