Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe (kushoto) akiwa amekabwa roba na mchezaji wa timu ya jeshi JKT Ruvu, George Osei (kulia).
Na Wilbert Molandi /CHAMPIONI MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amissi Tambwe, ameweka wazi kwamba mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting ambayo walimaliza kwa suluhu juzi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, haikuwa ya soka na yeye alinusurika kuuawa.
Tambwe amesema ni mechi itakayobaki kwenye kichwa chake kwa mambo mawili, kwanza ni beki George Osei ‘beki mkatili’ ambaye alimpiga kiwiko kwenye jicho na mdomoni.
Pili ni maneno makali yaliyoupasua moyo wake baada ya kuitwa mkimbizi na kukumbushiwa vita ya wenyewe kwa wenyewe inayoendelea nchini Burundi.
Katika mahojiano na Championi Jumatatu, Tambwe amesema Michael alimkaba kwa nguvu zaidi ya mara moja na kumfanya ashindwe kupumua.
“Haukuwa mpira, hauwezi kuamini kama kweli wale walikuja uwanjani kucheza soka. Walinipiga kiwiko, wakanipiga ngumi na mwisho Michael alinikaba shingoni zaidi ya mara moja na kunifanya nishindwe kupumua.
“Hii ni hatari, kuna mtu anaweza kuanguka akapoteza maisha siku moja. Wale wanajeshi hawaingii uwanjani kucheza soka, wanakwenda kucheza na mwili wa wachezaji wenzao.
“Ila nilishangazwa na mwamuzi kutoa kadi kwetu huku akionekana kuwahofia wanajeshi. Ukimwambia mwamuzi anachekacheka tu, sijui alikuwa anamaanisha nini.
“Nafikisha hata mashitaka kwa TFF, wawaangalie waamuzi na kuwasisitiza wafanye kazi yao kwa haki na kuwalinda wachezaji waliokwenda kucheza soka na si ugomvi,” alisema Tambwe na kuongeza.
“Kilichoniuma zaidi ni matusi na kuitwa mkimbizi, tena wakisema nimekimbia vita Burundi. Nimevumilia sana, ajabu wale ni askari lakini hawaonyeshi kuwa wanajua athari za vita.
“Sijalala, daktari wa timu aliniandikia dawa ya maji, nikaweka jichoni na pia ya kunywa. Bado jicho halioni vizuri.
“Halafu si mimi tu, hata (Kpah) Sherman walimpiga kibao usoni, akashangaa kama soka Tanzania linachezwa hivi!
“Sijawahi kutamka hata siku moja, lakini leo ninatamka kuwa soka la hapa nchini hivi sasa ni vita na siyo burudani tena, haiwezekani mchezaji anacheza soka huku akirusha ngumi, viwiko na mateke uwanjani huku mwamuzi akiangalia tu bila ya kutoa maamuzi yoyote.
“Pia ninamshangaa huyu jezi namba 4 (George Osei), yeye kila ninapokutana naye lazima acheze kwa kunipania kwa kunichezea rafu za makusudi, kunirushia ngumi na viwiko, sasa angalia kama leo kanipasua mdomoni na jicho linaanza kuvimba, hapa ninapoongea na wewe nashindwa kuona mbele vizuri,” alisema Tambwe kwa masikitiko makubwa na kuomba TFF kuchukua hatua zinazostahili kwa mchezaji huyo ili kurejeshe nidhamu mpirani.
MSIBA: MWIGIZAJI MAARUFU MUNA OBIEKWE AFARIKI DUNIA!
===>>SOMA ZAIDI HAPA! JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.
===>>SOMA ZAIDI HAPA!
KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO
TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142
(PICHA: MUSA MATEJA/GPL)

0 comments:
Post a Comment