KWAPA LA MPENZI WANGU LINANUKA ....!! KILA TUFANYAPO MAPENZI NI LAZIMA NIPIGE CHAFYA SANA...USHAURI JAMANI NIFANYAJE?

Mambo vipi Mdau Mtata?!
Mimi ni mdada mwenye umri wa miaka 27.Nina uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwenye umri wa miaka 33 kwa muda wa miezi mitano sasa.

Tatizo langu ni kuwa kila tufanyapo mapenzi huwa nashikwa na chafya kali sana.Chanzo chake ni kwapa ya mpenzi wangu ..

Nashindwa kuelewa tatizo ni nini maana kwenye suala la usafi sijaona kama ni tatizo kwake.Kabla ya tendo huwa tunaoga pamoja na humsugua sana tu..

Tukishafika kitandani kwapa hutoa harufu utadhani hajaoga mwezi mzima, yaani hata hamu ya tendo huniishia, kuziba pua nashindwa, nikihofia kwamba atanielewa vibaya.Kwa hiyo huwa navumilia tu ili mradi amalize hamu yake...

Jamani, naombeni msaada ili uhusiano wangu usivunjike maana bado nampenda mpenzi wangu.
Madam A.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment