MAKAVU LIVE: UCHAFU WA WANAWAKE WAMKERA JOHARI WA BONGO MOVIE...!

Staa wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
SOMO! Staa wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’, ametoa somo kwa baadhi ya wasanii wa kike ambao wamekuwa wakijibweteka na kushindwa kudumisha upendo kwa wapenzi wao baada ya kujifungua.

Akipiga stori na paparazi wetu, Johari alisema miongoni mwa vitu ambavyo huwashushia upendo wanawake wengi ni uchafu baada ya kuzaa na kujikita na malezi kuliko kuwathamini wapenzi wao ndiyo maana ameamua kutoa filamu ya Mke Mchafu inayowagusa mabinti.

“Ujue kuna watu wanavunja ndoa zao kwa mikono yao wenyewe kutokana na mambo kama haya na wapo hata wasanii ambao wanafanya haya mambo, yaani mtu unaingia kwenye nyumba hutamani hata kuomba maji ya kunywa, nafikiri watabadilika kupitia filamu yangu itakayotoka soon,” alisema Johari.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment