HATARI SANA: GARI LA IKULU YA KENYA LILIVYOIBWA LICHA YA KUWA NA ULINZI MKUBWA!

Ni moja kati ya zile stori za nadra sana kuzisikia yani, kwa uoga au ulinzi mkali ambao huwa unawekwa kwenye vitu vya serikali tena sehemu kama Ikulu ni nadra sana kusikia kuna jamaa wamejihami na kuiba.

Labda inawezekana hawa jamaa hawakuwa wanajua kama ni gari la Ikulu, aliekua analiendesha ni Askari akielekea kwenye makazi ya Askari lakini ghafla barabarani Nairobi akavamiwa na watu watatu waliokua na silaha aina ya AK 47.

Ilikua saa mbili usiku ambapo walimshusha wakamvua nguo na kumtupa kwenye mtaro alafu wakaondoka na gari ambalo ni miongoni mwa magari machache ya Ikulu yasiyopenya risasi.

Ni gari aina ya BMW ambalo huwa linakuwepo kwenye msafara wa Rais Uhuru Kenyatta ambapo kweli Ikulu imethibitisha gari hilo kuwa lake na kwamba msako wa kulitafuta na waliohusika pia unaendelea. – Manoa Esipisu msemaji wa Ikulu.
Share on Google Plus

About Anonymous

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment